Mariamu Ampaka Yesu Mafuta

12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alikwenda mpaka Bethania ambako Lazaro aliyemfufua alikuwa anaishi. Wakamwan dalia karamu; na Martha akawahudumia. Lazaro alikuwa miongoni mwa wageni waliokaa mezani pamoja na Yesu. Kisha Mariamu akachukua chupa yenye manukato ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu ya manukato. Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi, ambaye baadaye alimsaliti Yesu, akasema, “Kwa nini manukato haya hay akuuzwa zikapatikana fedha nyingi wapewe maskini?” Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. Yesu akajibu, “Msimsumbue! Mwacheni ayaweke manukato hayo kwa ajili ya siku ya kifo changu. Maskini wapo pamoja nanyi siku zote ila hamtakuwa nami siku zote. ” Umati mkubwa wa Wayahudi waliposikia kwamba Yesu ali kuwa Bethania, walikuja ili pia wamwone Lazaro ambaye alimfufua. 10 Kwa hiyo makuhani wakuu wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11 kwa kuwa baada ya kufufuliwa kwake Wayahudi wengi wal iamua kuwakataa viongozi wao na kumwamini Yesu.

Yesu Aingia Yerusalemu Akishangiliwa

12 Kesho yake watu wengi waliokuja mjini kwa sikukuu waka pata habari kuwa Yesu angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumpokea, huku wakiimba, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu ambar iki Mfalme wa Israeli!” 14 Yesu akampata mwanapunda akampanda, kama ilivyoandikwa katika Maandiko, 15 “Usiogope, wewe mwenyeji wa Sioni. Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!”

16 Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa mambo haya wakati huo, lakini Yesu alipofufuka kwa utukufu walikumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yametajwa katika Maandiko; na kwamba waliyatekeleza kwa ajili yake. 17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua, baadaye waliwasimulia wengine yaliy otokea. 18 Ndio sababu watu wengi walitoka kwenda kumpokea, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu. 19 Mafarisayo walipoona haya wakaambiana, “Mnaona? Hakuna tun aloweza kufanya; ulimwengu wote unamfuata!”

Yesu Anatabiri Kifo Chake

20 Kati ya watu waliokwenda Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu walikuwepo Wagiriki kadhaa. 21 Hawa walimjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, na wote wawili wakamwambia Yesu. 23 Yesu akawaambia, “Wakati umefika wa mimi Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24 Ninawaha kikishia kuwa, mbegu ya ngano isipopandwa ardhini na kufa, huba kia peke yake. Lakini ikifa inazaa nafaka kwa wingi. 25 Mtu ye yote anayeishi kwa ajili ya nafsi yake tu, ataipoteza, lakini mtu anayeishi kwa ajili ya wengine, atasalimisha nafsi yake kwa maisha ya milele. 26 Mtu ye yote anayetaka kunitumikia lazima anifuate; ili mtumishi wangu awepo mahali nilipo; na mtu ye yote akinitumikia, Baba yangu atampa tuzo ya heshima.

27 “Moyo wangu unafadhaika sana. Niombeje? ‘Baba uniepushe na mambo yatakayotokea’? La, nilikuja ulimwenguni kwa sababu hii. 28 Baba, dhihirisha utukufu wa jina lako!” Kisha ikasikika sauti kutoka mbinguni, “Nimedhihirisha utukufu wa jina langu, na nitafanya hivyo tena.” 29 Umati wa watu uliposikia sauti hii, baadhi walidhani ilikuwa ni sauti ya radi, na wengine wakasema, “Malaika alikuwa anaongea naye.” 30 Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika, si kwa faida yangu, bali ni kwa faida yenu. 31 Wakati wa Mungu kutamka hukumu juu ya ulimwengu umetimia, huu ni wakati ambao shetani, mtawala wa dunia hii, atapinduliwa. 32 Nami nitakapoinuliwa kutoka ardhini, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Alisema haya ili kuonyesha jinsi atakavyokufa. 34 Wakamwambia, “Tumesoma katika Maandiko ya sheria kuwa Kristo anaishi milele na hatakufa. Mbona unasema lazima Mwana wa Adamu ainuliwe? Huyo Mwana wa Adamu ni nani? 35 Yesu akawajibu, “Nuru yangu itawaangazia kwa muda mfupi. Tembeeni wakati nuru bado ipo nanyi msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui ana kokwenda. 36 Wakati mkiwa na nuru, muitegemee hiyo nuru ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka akajificha.

Kutokuamini Kwa Wayahudi

37 Hata baada ya miujiza yote Yesu aliyofanya mbele yao hawakumwamini. 38 Ikawa kama alivyotabiri nabii Isaya aliposema, “Bwana, ni nani ameamini tuliyowaambia? Na ni nani ambaye ameona nguvu za Bwana?” 39 Kwa hiyo hawakuamini, kwa sababu kama Isaya alivyosema tena, 40 “Mungu amewafanya vipofu wasione na mioyo yao ameifanya migumu, ili wasije wakaona kwa macho yao na kuamini kwa mioyo yao, na kumgeukia Mungu awaponye.” 41 Isaya alisema haya kwa kuwa aliona katika maono utukufu wa Yesu na akatabiri juu yake. 42 Hata hivyo wapo wengi, pamoja na viongozi wa Way ahudi, ambao walimwamini, lakini hawakukiri wazi wazi kwa sababu waliwaogopa Mafarisayo, wasije wakafukuzwa kutoka katika masina gogi yao. 43 Wao walithamini zaidi sifa za watu kuliko sifa kutoka kwa Mungu.

Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani

44 Yesu akasema kwa sauti kuu, “Mtu anayeniamini mimi, anamwamini Mungu aliyenituma. 45 Na mtu anayeniona mimi, anam wona yeye ali yenituma. 46 Nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu anayeniamini asibaki gizani. 47 Mtu anayesikia maneno yangu asiyatii, simhukumu; kwa maana sikuja ulimwenguni kuhukumu bali kuokoa. 48 Mtu anayenikataa na kuyapuuza maneno yangu anaye hakimu; neno nililotamka litamhukumu siku ya mwisho. 49 Sikusema mambo haya kwa mamlaka yangu mwenyewe. Bali Baba yangu aliyeni tuma amenipa amri kuhusu mambo ninayosema na kutamka. 50 Ninafa hamu ya kuwa sheria yake ni uzima wa milele. Kwa hiyo ninayosema ni yale ambayo Baba yangu ameniagiza niyaseme.”

Mwanamke Ampa Yesu Heshima

(Mt 26:6-13; Mk 14:3-9)

12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alienda Bethania. Huko ndiko alikoishi Lazaro, yule mtu aliyefufuliwa na Yesu kutoka wafu. Hapo walimwandalia Yesu karamu ya chakula. Naye Martha alihudumu na Lazaro alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakila chakula pamoja na Yesu. Mariamu akaleta manukato ya thamani sana yaliyotengenezwa kwa nardo asilia kwenye chombo chenye ujazo wa nusu lita[a] hivi. Akayamwaga manukato hayo miguuni mwa Yesu. Kisha akaanza kuifuta miguu ya Yesu kwa nywele zake. Harufu nzuri ya manukato hayo ikajaa nyumba nzima.

Yuda Iskariote, mmoja wa wafuasi wa Yesu, naye alikuwepo hapo. Yuda ambaye baadaye angemkabidhi Yesu kwa maadui zake akasema, “Manukato hayo yana thamani ya mshahara wa mwaka[b] wa mtu. Bora yangeuzwa, na fedha hizo wangepewa maskini.” Lakini Yuda hakusema hivyo kwa vile alikuwa anawajali sana maskini. Alisema hivyo kwa sababu alikuwa mwizi. Naye ndiye aliyetunza mfuko wa fedha za wafuasi wa Yesu. Naye mara kadhaa aliiba fedha kutoka katika mfuko huo.

Yesu akajibu, “Msimzuie. Ilikuwa sahihi kwake kutunza manukato haya kwa ajili ya siku ya leo; siku ambayo maziko yangu yanaandaliwa. Nyakati zote mtaendelea kuwa pamoja na hao maskini.[c] Lakini si kila siku mtakuwa pamoja nami.”

Mpango Dhidi ya Lazaro

Wayahudi wengi wakasikia kwamba Yesu alikuwa Bethania, Kwa hiyo walienda huko ili wakamwone. Walienda pia ili kumwona Lazaro, yule ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu. 10 Viongozi wa makuhani nao wakafanya mpango wa kumuua Lazaro. 11 Walitaka kumwua kwa sababu, Wayahudi wengi waliwaacha makuhani hao na kumwamini Yesu.

Yesu Anaingia Yerusalemu Kama Mfalme

(Mt 21:1-11; Mk 11:1-11; Lk 19:28-40)

12 Siku iliyofuata watu waliokuwamo Yerusalemu walisikia kwamba Yesu alikuwa anakuja huko. Hili ni kundi la watu waliokuja kusherehekea sikukuu ya Pasaka. 13 Hawa walibeba matawi ya miti ya mitende na kwenda kumlaki Yesu. Pia walipiga kelele wakisema,

“‘Msifuni[d] Yeye!’
‘Karibu! Mungu ambariki yeye
    ajaye kwa jina la Bwana!’(A)
Mungu ambariki Mfalme wa Israeli!”

14 Yesu akamkuta punda njiani naye akampanda, kama vile Maandiko yanavyosema,

15 “Msiogope, enyi watu wa Sayuni![e]
Tazameni! Mfalme wenu anakuja.
    Naye amepanda mwana punda.”(B)

16 Wafuasi wa Yesu hawakuyaelewa yale yaliyokuwa yanatokea wakati huo. Lakini Yesu alipoinuliwa juu kwenye utukufu, ndipo walipoelewa kuwa haya yalitokea kama ilivyoandikwa juu yake. Kisha wakakumbuka kwamba walifanya mambo haya kwa ajili ya Yesu.

17 Siku Yesu alipomfufua Lazaro kutoka wafu na kumwambia atoke kaburini walikuwepo watu wengi pamoja naye. Hawa walikuwa wakiwaeleza wengine yale aliyoyafanya Yesu. 18 Ndiyo sababu watu wengi walienda ili kumlaki Yesu; kwa kuwa walikuwa wamesikia habari za ishara hii aliyoifanya. 19 Mafarisayo nao wakasemezana wao kwa wao, “Tazameni! Mpango wetu haufanyi kazi. Watu wote wanamfuata Yesu!”

Yesu Azungumza Juu Uzima na Kifo

20 Hapo Yerusalemu walikuwepo pia Wayunani. Hawa walikuwa ni miongoni mwa watu walioenda mjini humo kuabudu wakati wa sikukuu ya Pasaka. 21 Hao walimwendea Filipo, aliyetoka Bethsaida kule Galilaya. Wakasema, “Bwana, tunahitaji kumwona Yesu.” 22 Filipo alienda na kumwambia Andrea hitaji lao. Kisha Andrea na Filipo walienda na kumwambia Yesu.

23 Yesu akawaambia Filipo na Andrea, “Wakati umefika kwa Mwana wa Adamu kuupokea utukufu wake. 24 Ni ukweli kwamba mbegu ya ngano inapaswa kuanguka katika ardhi na kuoza kabla ya kukua na kuzaa nafaka nyingi ya ngano. Kama haitakufa, haitaongezeka zaidi ya hiyo mbegu moja. 25 Yeyote anayeyapenda maisha yake aliyonayo atayapoteza. Yeyote atakayetoa maisha yake kwa Yesu katika ulimwengu huu atayatunza. Nao wataupata uzima wa milele. 26 Kama mtu atanitumikia inampasa anifuate. Watumishi wangu watakuwa pamoja nami popote nitakapokuwa. Mtu atakayenitumikia Baba yangu atamheshimu.

Yesu Azungumza Kuhusu Kifo Chake

27 Sasa ninapata taabu sana rohoni mwangu. Nisemeje? Je, niseme, ‘Baba niokoe katika wakati huu wa mateso’? Hapana, nimeufikia wakati huu ili nipate mateso. 28 Baba yangu, ufanye yale yatakayokuletea wewe utukufu!”

Kisha sauti kutoka mbinguni ikasikika ikisema, “Tayari nimekwisha upata utukufu wangu. Nitaupata tena.”

29 Watu waliokuwa wamesimama hapo wakaisikia sauti hiyo. Wakasema ilikuwa ni ngurumo. Lakini wengine wakasema, “Malaika amesema naye!”

30 Yesu akasema, “Sauti hiyo ilikuwa ni kwa ajili yenu si kwa ajili yangu. 31 Sasa ni wakati wa ulimwengu kuhukumiwa. Sasa mtawala wa ulimwengu[f] huu atatupwa nje. 32 Nami nitainuliwa juu[g] kutoka katika nchi. Mambo hayo yatakapotokea, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Yesu alisema hili kuonesha jinsi ambavyo atakufa.

34 Watu wakasema, “Lakini sheria yetu inasema kwamba Masihi ataishi milele. Sasa kwa nini unasema, ‘Ni lazima Mwana wa Adamu ainuliwe juu’? Ni nani huyu ‘Mwana wa Adamu’?”

35 Kisha Yesu akasema, “Nuru[h] itabaki pamoja nanyi kwa muda mfupi tu. Kwa hiyo mtembee mkiwa bado na hiyo nuru. Hapo giza[i] halitaweza kuwakamata. Watu wanaotembea gizani hawajui kule wanakoenda. 36 Hivyo wekeni matumaini yenu katika nuru wakati bado mkiwa nayo. Jinsi hiyo mtakuwa watoto wa nuru.” Yesu alipomaliza kusema mambo hayo, aliondoka na kwenda mahali ambapo watu wasingeweza kumwona.

Baadhi ya Wayahudi Wakataa Kumwamini Yesu

37 Watu wakaona ishara[j] hizi zote alizozifanya Yesu, lakini bado hawakumwamini. 38 Haya yalikuwa hivyo ili kuthibitisha yale aliyoyasema nabii Isaya kuwa:

“Bwana, ni nani aliyeamini yale tuliyowaambia?
    Ni nani aliyeziona nguvu za Bwana?”(C)

39 Hii ndiyo sababu watu hawakuweza kuamini. Kwani Isaya alisema pia,

40 “Mungu aliwafanya baadhi ya watu wasione.
    Aliufunga ufahamu wao.
Alifanya hivi ili wasiweze kuona kwa macho yao
    na kuelewa kwa ufahamu wao.
Alifanya hivyo ili wasiweze kugeuka
    na kuponywa.”(D)

41 Isaya alisema hivi kwa sababu aliuona ukuu wa Mungu[k] ndani ya Yesu. Naye alizungumza habari zake Yesu.

42 Lakini watu wengi wakamwamini Yesu. Hata wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi wakamwamini, lakini walikuwa na hofu juu ya Mafarisayo, hivyo hawakusema kwa uwazi kwamba wameamini. Hao walikuwa na hofu kwamba wangeamriwa watoke na kukaa nje ya sinagogi. 43 Wao walipenda kusifiwa na watu zaidi kuliko kupata sifa zinazotoka kwa Mungu.

Mafundisho ya Yesu Yatawahukumu Watu

44 Kisha Yesu akapaza sauti, “Mtu yeyote anayeniamini basi kwa hakika anamwamini yule aliyenituma. 45 Yeyote anayeniona mimi hakika anamwona yeye aliyenituma. 46 Nimekuja katika ulimwengu huu kama mwanga. Nimekuja ili kila mmoja atakayeniamini asiendelee kuishi katika giza.

47 Sikuja ulimwenguni humu kuwahukumu watu. Nimekuja ili kuwaokoa watu wa ulimwengu huu. Hivyo mimi siye ninayewahukumu wale wanaosikia mafundisho yangu bila kuyafuata. 48 Isipokuwa yupo hakimu wa kuwahukumu wote wanaokataa kuniamini na wasiokubaliana na yale ninayoyasema. Ujumbe ninaousema utawahukumu ninyi siku ya mwisho. 49 Hiyo ni kwa sababu yale niliyofundisha hayakutoka kwangu. Baba aliyenituma ndiye aliyeniambia yale nitakayosema na kuyafundisha. 50 Nami najua amri za Mungu kwamba lolote alisemalo na kutenda litawaletea watu uzima wa milele, kama watazifanya. Hivyo mambo ninayosema ni yale ambayo Baba yangu ameniambia niyaseme.”

Footnotes

  1. 12:3 nusu lita Kwa maana ya kawaida, “litra” ni ratili ya Kirumi, sawa na gramu 327.
  2. 12:5 mshahara wa mwaka Wa mwaka wa mtu kwa hali halisi “dinari 300” (sarafu za fedha). Sarafu moja, dinari ya Kirumi, ilikuwa ni wastani wa mshahara wa mtu wa siku moja.
  3. 12:8 maskini Nyakati zote wataendelea kuwepo maskini pamoja nanyi. Tazama Kum 15:11.
  4. 12:13 Msifuni Kwa maana ya kawaida, “Hosanna”, ambalo ni neno la Kiebrania lililotumika kumwomba msaada Mungu. Hapa, labda ilikuwa ni kelele ya shangwe iliyotumika kumsifu Mungu au Masihi wake.
  5. 12:15 watu wa Sayuni Kwa maana ya kawaida, “binti Sayuni”, ina maana mji wa Yerusalemu. Tazama Sayuni kwenye Orodha ya Maneno.
  6. 12:31 mtawala wa ulimwengu Huyu ni Shetani. Tazama Shetani katika Orodha ya Maneno.
  7. 12:32 nitainuliwa juu Hapa “Kuinuliwa juu” ina maana ya kupigiliwa misumari msalabani na “kuinuliwa” nao. Pia katika mstari wa 34.
  8. 12:35 Nuru Ina maana ya Kristo, kama katika Yh 1:5-9. Pia ni ishara ya wema na kweli unahusiana na Kristo na ufalme wake.
  9. 12:35 giza Giza au usiku ni ishara ya aina zote za mambo yanayoueleza ufalme wa Shetani, kama vile dhambi na maovu.
  10. 12:37 ishara Ni tendo la kushangaza linalodhihirisha nguvu za Mungu.
  11. 12:41 Mungu Kihalisia, “utukufu”, ni neno linaloonyesha sifa maalumu za Mungu. Tazama Utukufu katika Orodha ya Maneno.