Yesu Anatabiri Kubomolewa Kwa Hekalu

13 Alipokuwa akitoka nje ya Hekalu, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, ona jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo maridadi!”

Yesu akamjibu, “Unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomo lewa.”

Yesu Anawaambia Wafuasi Wake Wajiandae Kwa Mateso

Alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni akiliangalia Hekalu, Petro, Yakobo na Yohana walimwuliza faraghani, “Tafadhali tuambie, mambo haya yatatokea lini, na ni ishara gani zitaonyesha kuwa karibu yatatimia?” Yesu akaanza kuwaeleza: “Jihadharini mtu asije akawadanganya. Wengi wata kuja wakilitumia jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye’ na wata wadanganya wengi. Na mkisikia habari za vita na uvumi juu ya vita, msishtuke. Mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho utakuwa bado. Mataifa yatapigana na falme kushambuliana. Matetemeko ya ardhi yatatokea sehemu mbalimbali na kutakuwa na njaa. Lakini huu utakuwa kama maumivu ya mwanzo tu ya uchungu wa uzazi. Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watu watawapeleka mahakamani na mtapigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ndipo mtaweza kutoa ushuhuda kuhusu Habari Njema. 10 Lakini kabla mwisho kufika, Habari Njema itahubiriwa kwa mataifa yote. 11 “Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.

12 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 13 Kila mtu atawachukia kwa ajili yangu; lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.

14 “Mtakapoona ile ‘sanamu ya chukizo’ imesimama mahali isipostahili - msomaji na aelewe maana yake -basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 15 Mtu aliyeko juu ya nyumba asiter emke kuingia ndani kuchukua cho chote. 16 Aliyeko shambani asi rudi nyumbani kuchukua koti lake. 17 Ole wao akina mama waja wazito na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 18 Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa masika. 19 Kwa maana siku hizo itaku wapo dhiki kuu ambayo haijapata kutokea tangu dunia ilipoumbwa, wala haitatokea tena. 20 Na kama Bwana hakuufupisha muda huo wa dhiki, hakuna mtu ambaye angesalimika; lakini kwa ajili ya watu wake aliowachagua, ameufupisha muda huo.

21 “Na wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa’ au , ‘Tazama, yule pale,’ msiamini. 22 Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watafanya ishara na miujiza ili kuwadanganya hata wale waliochaguliwa na Mungu, kama ikiwezekana. 23 Kwa hiyo jihadharini kwa maana nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea.”

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

24 “Siku hizo, baada ya hiyo dhiki, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake. 25 Nyota zitaanguka kutoka mbinguni na nguvu za anga zitatikisika. 26 Ndipo watu wote wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utu kufu. 27 Nami nitawatuma malaika wawakusanye watu wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa nchi hadi mwisho wa mbi ngu.

28 “Sasa jifunzeni jambo hili kutoka kwa mtini: mwonapo matawi ya mtini yakianza kulainika na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29 Hali kadhalika mtaka poyaona mambo haya yanatokea, tambueni kwamba mimi Mwana wa Adamu, ni karibu kuja. 30 Ninawaambieni hakika, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo haya kutokea. 31 Mbingu na nchi zita toweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

32 “Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake. 33 “Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi. Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36 Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37 Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”

Yesu Aonya Kuhusu Wakati Ujao

(Mt 24:1-25; Lk 21:5-24)

13 Yesu alikuwa akiondoka katika eneo la Hekalu na moja ya wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, tazama mawe haya yanavyopendeza na jinsi majengo haya yanavyopendeza!”

Yesu akamjibu, “Je, mnayaona majengo haya makubwa? Yote yatabomolewa. Kila jiwe litaporomoshwa hata chini. Hakuna jiwe lolote kati ya haya litakaloachwa mahali pake.”

Naye alipokuwa ameketi juu ya Mlima wa Mizeituni upande wa pili kuvuka Hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea walimwuliza wakiwa faragha, “Haya tuambie, ni lini mambo haya yatakapotokea? Ni ishara gani itakayoonesha ya kwamba yote yanakaribia kutimizwa?”

Yesu akaanza kuwaeleza, “Muwe waangalifu mtu asije akawadanganya. Wengi watakuja huku wakilitumia Jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye Masihi,’[a] nao watawadanganya wengi. Mtasikia juu ya vita vinavyopiganiwa na mtasikia habari juu ya vita vingine vinavyoanza. Hata hivyo msishtushwe. Mambo hayo lazima yatokee, kabla ule mwisho wenyewe kufika. Kwani taifa moja litapigana dhidi ya taifa lingine na ufalme mmoja utapigana dhidi ya ufalme mwingine. Yatatokea matetemeko mengi mahali pengi na kutakuwepo na njaa kali sehemu nyingi. Mambo haya yatakuwa ni mwanzo tu wa uchungu wa mama mzazi kabla ya mtoto kuzaliwa.

Hivyo mjihadhari! Wapo watu watakaowakamata na kuwapeleka mkahukumiwe kwa kuwa ninyi ni wanafunzi wangu. Watawapiga katika masinagogi yao. Mtalazimishwa kusimama mbele ya wafalme na watawala. Nanyi mtawaeleza habari zangu. 10 Kabla ya mwisho kufika, ni lazima kwanza habari Njema itangazwe kwa mataifa yote. 11 Wakati wowote watakapowakamata na kuwashitaki, msiwe na wasiwasi kujiandaa kwa yale mtakayoyasema, lakini myaseme yale mtakayopewa saa ile ile, kwa kuwa si ninyi mnaozungumza; bali, ni Roho Mtakatifu anayezungumza.

12 Na ndugu atamsaliti nduguye hata kuuawa, na baba atamsaliti mwanawe. Watoto nao watawaasi wazazi wao na hata kuwatoa wauawe. 13 Nanyi mtachukiwa na wote kwa sababu yangu. Lakini yeyote atakayevumilia hadi mwisho ataokoka.

14 Wakati mtakapoliona chukizo la uharibifu[b] likisimama mahali pasipotakiwa lisimame.” (Msomaji aelewe hii ina maana gani?[c]) “Kisha wale waliopo katika Uyahudi wakimbilie milimani. 15 Ikiwa mtu yupo katika paa la nyumba yake, asishuke chini na kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu chochote. 16 Ikiwa mtu yupo shambani asirudi kuchukua vazi lake.

17 Wakati huo itakuwa hatari kwa wanawake walio waja wazito na wale wenye watoto wachanga. 18 Ombeni kwamba haya yasitokee wakati wa majira ya baridi. 19 Kwa kuwa taabu itakayotokea katika siku hizo itakuwa ile ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo pale Mungu alipoumba dunia hadi sasa. Na hakitatokea tena kitu kama hicho. 20 Kama Bwana asingelifupisha muda huo, hakuna ambaye angenusurika. Lakini yeye amefupisha siku hizo kwa ajili ya watu wale aliowateuwa.

21 Ikiwa mtu atawaambia, ‘Tazama, Kristo ni huyu hapa!’ ama ‘Ni yule pale!’ Usiliamini hilo. 22 Kwani Makristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea, nao watafanya ishara na miujiza kuwadanganya watu ikiwezekana hata wale ambao Mungu amewachagua. 23 Kwa hiyo mjihadhari nimewaonya juu ya mambo haya kabla hayajatokea.

Yesu Atakaporudi Tena

(Mt 24:29-51; Lk 21:25-36; 19:12-13,40)

24 Lakini katika siku hizo, baada ya kipindi cha dhiki,

‘Jua litatiwa giza,
    mwezi hautatoa mwanga,
25 nyota zitaanguka kutoka angani,
    na mbingu yote itatikisika.’[d]

26 Ndipo watu watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu kubwa na utukufu. 27 Baada ya hapo Mwana wa Adamu atawatuma malaika, na atawakusanya wateule wake kutoka kila upande wa dunia.

28 Jifunzeni somo hili kutoka katika mti wa mtini: Matawi yake yanaponyauka na kubeba majani, unajua kwamba kiangazi kimekaribia. 29 Vivyo hivyo, unapoona mambo haya yanaanza kutokea unajua kwamba muda umekaribia na umeshafika mlangoni. 30 Ninawaambieni ukweli: Kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo haya yote hayajatokea. 31 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

32 Hakuna anayejua wakiwemo malaika wa mbinguni ama Mwana bali baba peke yake lini siku au saa ile itakapowadia. 33 Mjihadhari; Kesheni! Kwani hamjui lini muda huo utafika.

34 Ni kama mtu anayeenda safarini na kabla ya kuondoka huiacha nyumba yake mikononi mwa watumishi wake. Kabla ya kuiacha nyumba yake anawaweka watumishi wake kusimamia kila mmoja akiwa na kazi yake maalumu. Kisha atamwamuru mlinzi mlangoni awe macho. 35 Vivyo hivyo ni lazima mjihadhari, kwa sababu hamjui ni muda gani mkuu wa nyumba atakuja; hamjui kama atakuja jioni, usiku wa manane, wakati jogoo anawika, au alfajiri. 36 Ikiwa atakuja ghafula, basi asiwakute mmelala. 37 Ninachowaambia, namwambia kila mmoja: ‘muwe tayari.’”

Footnotes

  1. 13:6 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Yule ambaye”, kwa maana ya Mfalme Mteule wa Mungu aliyetumwa na Mungu. Tazama Mt 24:5 na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 13:14 chukizo la uharibifu Ni maneno yanayoashiria kitu ambacho Mungu hapendezwi nacho. Tazama Dan 9:27; 11:31 na 12:11.
  3. 13:14 Msomaji aelewe hii ina maana gani Mwandishi anamtaka msomaji azingatie kwamba anazungumzia Jeshi la Rumi ambalo litaharibu Yerusalemu, ingawa hataki kulielezea hili kwa wazi. Tazama Lk 21:20-24.
  4. 13:24-25 Tazama Isa 13:10; 34:4.