Add parallel Print Page Options

12 Akasema, “Mtu mmoja maarufu alikuwa anajiandaa kwenda katika nchi ya mbali kutawazwa kuwa mfalme. Kisha arudi nyumbani na kuwatawala watu wake. 13 Hivyo aliwaita watumishi wake kumi kwa pamoja. Akampa kila mtumishi fungu la pesa.[a] Akamwambia kila mtumishi, ‘Zifanyie biashara pesa hizi mpaka nitakaporudi.’

Read full chapter

Footnotes

  1. 19:13 fungu la pesa Fungu moja la pesa kwa Kiyunani liliitwa mina, ambayo ni sarafu 100 za fedha, uliotosha kumlipa mtu mshahara kwa miezi mitatu. Pia katika mstari wa 16,18,20,24 na 25.