Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha

Baada ya haya, Yesu alikwenda tena Yerusalemu kuhudhuria sikukuu mojawapo ya Wayahudi. Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, pana bwawa moja ambalo kwa Kiebrania linaitwa Bethzatha ambalo lina baraza tano zenye safu za matao. Wagonjwa wengi sana, vipofu, viwete, na waliopooza walingojea kwenye baraza hizo. Walikuwa wakisubiri maji yatibuliwe, [ kwa maana malaika wa Bwana alikuja mara kwa mara akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia bwawani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wo wote aliokuwa nao.]

Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo alikuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona amelala hapo, na akijua kwamba amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, alimwul iza, “Unataka kupona?” Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine huniwahi akaingia kabla yangu.” Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako, utembee!” Mara moja yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea! Jambo hili lilitokea siku ya sabato. 10 Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni sabato. Huruhusiwi kubeba mkeka wako.”

11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chu kua mkeka wako utembee.”’

12 Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako utembee?”

13 Yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya kwa sababu palikuwa na umati mkubwa wa watu na Yesu alikuwa amepe nyezea humo akaondoka.

14 Baadaye Yesu alimkuta yule aliyemponya Hekaluni akamwam bia, “Sasa umepona. Angalia usitende dhambi tena usijepatwa na jambo baya zaidi.”

15 Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

16 Kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya sabato, wal ianza kumsumbua. 17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi pia sina budi kufanya mema.” 18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate kumwua, kwa sababu, zaidi ya kuvunja sheria za sabato, alikuwa akijifanya sawa na Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu.

Mamlaka Ya Mwana

19 Yesu akawajibu, “Ninawaambia hakika, Mwana hawezi kufa nya jambo lo lote mwenyewe isipokuwa lile alilomwona Baba yake akifanya; na lo lote alifanyalo Baba, Mwana pia hulifanya. 20 Kwa kuwa Baba anampenda Mwana na anamwonyesha mambo yote afa nyayo; pia atamwonyesha hata mambo makubwa kuliko haya, ambayo yatawastaajabisha. 21 Kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale awapendao. 22 Baba hamhukumu mtu ye yote, mamlaka ya kuhukumu amemwachia Mwana; 23 ili kila mtu amheshimu Mwana kama amheshimuvyo Baba. Ye yote anayekataa kumheshimu Mwana, anakataa kumheshimu Baba aliyemtuma. 24 Ninawaambia hakika, ye yote anayesikiliza maneno yangu na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Amevuka kutoka kwenye mauti, na kuingia katika uzima. 25 Nina waambia hakika, wakati utafika, tena umekwisha timia, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wote watakaoisikia wata kuwa hai. 26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha Mwanae kuwa chanzo cha uzima. 27 Na amempa Mwanae mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.

28 “Msishangae kusikia haya. Wakati unakuja ambapo wafu wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini; wale waliot enda mema watafufuka na kuwa hai, na wale waliotenda maovu, wata fufuka na kuhukumiwa. 30 Mimi siwezi kufanya jambo lo lote kwa mamlaka yangu mwenyewe. Mimi nahukumu kufuatana na jinsi Mungu anavyoniambia. Na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufa nya nipendavyo, bali nafanya mapenzi yake yeye aliyenipeleka.”

Mashahidi Wa Yesu

31 “Kama ningekuwa najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingekuwa na uzito. 32 Lakini yupo mwingine anishuhudiaye na ninafahamu kwamba ushuhuda wake ni wa kweli. 33 Mliwapeleka wajumbe wenu kwa Yohana, naye akashuhudia iliyo kweli. 34 Si kwamba ninategemea ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa. 35 Yohana alikuwa taa iliy owaka na kuwaangazia, na kwa muda mlikubali kufurahia nuru yake.

36 “Lakini ninao ushuhuda mzito zaidi kuliko wa Yohana. Kazi ambayo Baba amenituma nikamilishe, naam , ishara hizi nina zofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye aliyenituma. 37 Na Baba aliyenituma naye amenishuhudia. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuiona sura yake. 38 Wala ujumbe wake hamuupokei maana hamumwamini aliyemtuma.

39 “Mnasoma Maandiko kwa bidii kwa maana mnafikiri kuwa humo mtapata uzima wa milele. Maandiko hayo hayo ndio yanayonish uhudia mimi. 40 Lakini mnakataa kuja kwangu kupata uzima.

41 “Mimi sitafuti kutukuzwa na watu. 42 Lakini, ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu na mnakataa kunipokea. Lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. 44 Ndio maana hamwezi kuamini! Mnapenda sana kusifiana wenyewe kwa wenyewe wala ham jishughulishi kutafuta sifa kutoka kwake ambaye peke yake ndiye

Mungu!

45 “Msidhani kuwa mimi nitawashtaki kwa Baba. Anayewashtaki ni huyo Musa ambaye mnamwekea matumaini yenu. 46 Kama kweli mli kuwa mmemwamini Musa, mngaliniamini na mimi kwa maana aliandika kunihusu mimi. 47 Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Musa, mtaaminije ninayoyasema?”