Yesu Ajitambulisha Kwa Wanafunzi Saba

21 Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.

Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.

Yesu Amwuliza Petro Kama Anampenda

15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”

24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.

Yesu Awatokea wafuasi Wake Saba

21 Baadaye, Yesu akawatokea tena wafuasi wake karibu na Ziwa Galilaya. Hivi ndivyo ilivyotokea: Baadhi ya wafuasi wake walikuwa pamoja; Simoni Petro, Tomaso (aliyeitwa Pacha), Nathanaeli kutoka Kana kule Galilaya, wana wawili wa Zebedayo, na wafuasi wengine wawili. Simoni Petro akasema, “Ninaenda kuvua samaki.”

Wafuasi wengine wakasema, “Sisi sote tutaenda pamoja nawe.” Hivyo wote wakatoka na kwenda kwenye mashua. Usiku ule walivua lakini hawakupata kitu.

Asubuhi na mapema siku iliyofuata Yesu akasimama ufukweni mwa bahari. Hata hivyo wafuasi wake hawakujua kuwa alikuwa ni yeye Yesu. Kisha akawauliza, “Rafiki zangu, mmepata samaki wo wote?”

Wao wakajibu, “Hapana.”

Yesu akasema, “Tupeni nyavu zenu kwenye maji upande wa kulia wa mashua yenu. Nanyi mtapata samaki huko.” Nao wakafanya hivyo. Wakapata samaki wengi kiasi cha kushindwa kuzivuta nyavu na kuziingiza katika mashua.

Mfuasi aliyependwa sana na Yesu akamwambia Petro, “Mtu huyo ni Bwana!” Petro aliposikia akisema kuwa alikuwa Bwana, akajifunga joho lake kiunoni. (Alikuwa amezivua nguo zake kwa vile alitaka kufanya kazi.) Ndipo akaruka majini. Wafuasi wengine wakaenda ufukweni katika mashua. Wakazivuta nyavu zilizojaa samaki. Nao hawakuwa mbali sana na ufukwe, walikuwa kadiri ya mita 100[a] tu. Walipotoka kwenye mashua na kuingia kwenye maji, wakaona moto wenye makaa yaliokolea sana. Ndani ya moto huo walikuwemo samaki na mikate pia. 10 Kisha Yesu akasema leteni baadhi ya samaki mliowavua.

11 Simoni Petro akaenda kwenye mashua na kuvuta wavu kuelekea ufukweni. Wavu huo ulikuwa umejaa samaki wakubwa, wapatao 153 kwa ujumla! Lakini pamoja na wingi wa samaki hao, nyavu hazikukatika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mfuasi mmoja aliyemwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua yeye alikuwa ni Bwana. 13 Yesu akatembea ili kuchukua mikate na kuwapa. Akawapa samaki pia.

14 Hii sasa ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wafuasi wake baada ya kufufuka kutoka wafu.

Yesu Azungumza na Petro

15 Walipomaliza kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda kuliko watu wote hawa wanavyonipenda?”

Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, unajua kuwa nakupenda.”

Kisha Yesu akamwambia, “Wachunge wanakondoo[b] wangu.”

16 Kwa mara nyingine Yesu akamwambia, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?”

Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana, wewe unajua kuwa nakupenda.”

Kisha Yesu akasema, “Watunze kondoo wangu.”

17 Mara ya tatu Yesu akasema, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?”

Petro akahuzunika kwa sababu Yesu alimuuliza mara tatu, “Unanipenda?” Akasema, “Bwana, unafahamu kila kitu. Unajua kuwa nakupenda!”

Yesu akamwambia, “Walinde kondoo wangu. 18 Ukweli ni huu, wakati ulipokuwa mdogo, ulijifunga mwenyewe mkanda wako kiunoni na kwenda ulikotaka. Lakini utakapozeeka, utainyoosha mikono yako,[c] na mtu mwingine atakufunga mkanda wako. Watakuongoza kwenda mahali usikotaka kwenda.” 19 (Yesu alisema hivi kumwonyesha jinsi Petro atakavyokufa ili kumpa utukufu Mungu.) Kisha akamwambia Petro, “Nifuate!”

20 Petro akageuka na kumwona yule mfuasi mwingine aliyependwa sana na Yesu akitembea nyuma yao. (Huyu alikuwa ni mfuasi aliyejilaza kwa Yesu wakati wa chakula cha jioni na kusema, “Bwana, ni nani atakayekusaliti kwa maadui zako?”) 21 Petro alipomwona nyuma yao, akamwuliza Yesu, “Bwana, vipi kuhusu yeye?”

22 Yesu akajibu, “Labda nataka awe hai hadi nitakaporudi. Hilo wewe usilijali. Wewe nifuate!”

23 Kwa hiyo habari ikaenea miongoni mwa wafuasi wa Yesu. Wao walikuwa wakisema kuwa mfuasi huyo asingekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa asingekufa. Yeye alisema tu, “Labda nataka awe hai hadi nitakaporudi. Hilo wewe usilijali.”

24 Huyo mfuasi ndiye yeye anayesimulia habari hizi. Ndiye ambaye sasa ameziandika habari zote hizi. Nasi tunajua kuwa anayoyasema ni kweli.

25 Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu. Kama kila moja ya hayo yote yangeandikwa, nafikiri ulimwengu wote usingevitosha vitabu ambavyo vingeandikwa.

Footnotes

  1. 21:8 mita 100 Au “mikono 200”.
  2. 21:15 wanakondoo Yesu alitumia neno hili au neno “kondoo” katika mistari 16 na 17 ikimaanisha wafuasi wake, kama ilivyo katika Yh 10.
  3. 21:18 utainyoosha mikono yako Kunyoosha mikono ilikuwa no njia ya kawaida ya kusema juu ya kusulubishwa.