Mkristo Hafungwi Na Sheria

Ndugu zangu, kwa kuwa sasa ninasema na wale wanaoifahamu sheria, bila shaka mnaelewa kwamba mtu akifa hafungwi tena na sheria. Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa hufungwa kisheria kwa mumewe wakati wote mumewe akiwa hai. Lakini mumewe akifa mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa. Endapo mwanamke huyo ataishi namwanaume mwingine wakati mumewe yu hai, ataitwa mzinzi. Lakini mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na she ria ya ndoa, na akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

Kazi Ya Sheria

Kadhalika ndugu zangu, ninyi pia mmekufa kuhusu maagizo ya sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili tumzalie Mungu matunda. Tulipokuwa tukitawaliwa na hali yetu ya dhambi, tamaa zetu za dhambi zikiwa zinachochewa na sheria, zilikuwa zikifanya kazi katika miili yetu, tukatumikishwa katika huduma ya dhambi ambayo matunda yake ni kifo. Lakini sasa tumekuwa huru kutoka katika kifungo cha sheria kwa kuwa tumekufa kuhusu yale mambo yaliyotu funga, ili tuhudumu katika maisha mapya ya Roho na wala si katika ile njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.

Tusemeje basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, sivyo! Kama isingekuwapo sheria, nisingalifahamu dhambi ni nini. Hakika nisi ngalijua tamaa ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” Lakini dhambi ilipata nafasi katika amri hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi ime kufa. Kabla ya kuwapo sheria, nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipowasili dhambi nayo ilikuwa hai, nami nikafa. 10 Ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta kifo. 11 Dhambi ilipata nafasi katika amri, ikanidanganya, na kwa kutumia amri, ikaniletea kifo.

12 Kwa hiyo sheria yenyewe ni takatifu na amri ni takatifu, na ya haki, tena ni njema.

13 Je, hii ina maana kwamba sheria ambayo ni njema ilinile tea kifo? La, sivyo. Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, iliniletea kifo kwa njia ya sheria ambayo ni nzuri; kusudi kwa njia ya sheria, dhambi ionekane kuwa mbaya kabisa.

Mgongano Kati Ya Mwili Na Roho

14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu. Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya kazi mwilini mwangu.

24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo? 25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria ya dhambi.