Yesu Ni Mkuu Kuliko Musa

Kwa hiyo, ndugu zangu watakatifu, ambao mmeshiriki wito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na kuhani mkuu wa imani tunay oikiri.

Kwa maana Yesu alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemchagua, kama vile Musa alivyokuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu. Lakini Yesu amehesabiwa kuwa anastahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile mjenzi wa nyumba anavyopewa heshima zaidi kuliko nyumba aliyoijenga. Maana kila nyumba hujengwa na mtu fulani bali aliyejenga vitu vyote ni Mungu. Ni kweli kwamba Musa ali kuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, akishu hudia juu ya yale mambo ambayo Mungu angeyatamka baadaye, lakini Kristo alikuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu kama mwana. Na sisi ni nyumba yake, ikiwa tutashikilia ujasiri wetu na lile tumaini tunalojivunia.

Jihadharini Na Kutokuamini

Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama mlivyofanya wakati wa uasi , siku ile ya majaribio jangwani, ambapo baba zenu walinijaribu wakaona kazi zangu kwa miaka arobaini. 10 Kwa hiyo kizazi kile kilinikasirisha, nikasema, ‘Mioyo ya watu hao imepotoka; hawajapata kujua njia zangu.’ 11 Katika hasira yangu nikaapa, ‘Hawataingia kwenye pumziko langu kamwe.’

12 Angalieni, ndugu zangu, asiwepo miongoni mwenu mtu ye yote mwenye moyo wa dhambi, usioamini, unaomfanya ajitenge na Mungu wa uzima. 13 Bali muonyane kila siku maadamu bado ni ‘ ‘leo” ili asiwepo mtu kati yenu anayefanywa mkaidi na udangany ifu wa dhambi. 14 Kwa maana sisi ni washiriki pamoja na Kristo iwapo tutashikilia tumaini letu la kwanza kwa uaminifu mpaka mwisho. 15 Kama Maandiko yalivyosema: “Leo mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu. Kama mlivyofanya wakati wa uasi.” 16 Ni nani hao waliosikia lakini wakaasi? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17 Na ni nani waliom kasirisha Mungu kwa miaka arobaini? Si wale waliofanya dhambi wakafa jangwani? 18 Na ni nani ambao Mungu aliapa kuwa hawatain gia kwenye pumziko lake, isipokuwa wale waliokataa kutii? 19 Kwa hiyo tunaona kwamba walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Pumziko La Sabato