Sifa Za Kuhani Mkuu

Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa watu huteuliwa kumtumikia Mungu kwa niaba yao, kutoa sadaka na dhabihu kwa ajili ya dhambi zao. Anaweza kuwaonea huruma wale wasioel ewa na wanaopotoka kwa sababu yeye mwenyewe anasumbuliwa na udhaifu kama wao . Kwa sababu hii, anawajibika kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za hao watu.

Hakuna mtu anayejichagulia heshima hii ya kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huitwa na Mungu kama vile Haruni alivyoitwa.

Kristo hakujichagulia mwenyewe utukufu wa kuwa kuhani mkuu. Bali aliteuliwa na Mungu ambaye alimwambia, “Wewe ni mwanangu, leo hii nimekuzaa;” na tena kama asemavyo mahali pengine, “Wewe ni kuhani milele, katika ngazi ile ya ukuhani ya Mel kizedeki. Yesu alipokuwa akiishi duniani, alitoa dua na maombi kwa kilio kikuu na machozi kwa Mungu ambaye angeweza kumwokoa na kumtoa katika kifo, naye Mungu alimsikia kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na mtiifu. Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, aliji funza utii kutokana na mateso aliyopata; na baada ya kufanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii, 10 akateuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu wa ngazi ile ile ya

Onyo Kuhusu Kuanguka

11 Kuhusu ukuhani huu, tunayo mengi ya kusema ambayo ni mag umu kuyaeleza, kwa maana ninyi si wepesi wa kuelewa. 12 Ingawa kwa wakati huu mngalipaswa kuwa walimu, lakini bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za kwanza za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu. 13 Kwa maana anayeishi kwa maziwa peke yake bado ni mtoto mchanga, hana ujuzi katika mafund isho kuhusu neno la haki. 14 Bali chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, watu ambao wamekomaa akili kutokana na mafunzo ya mazoezi ya kupambanua kati ya mema na mabaya.

Kila kuhani Mkuu wa Kiyahudi alichaguliwa kutoka miongoni mwa watu. Kuhani huyo anapewa kazi ya kuwasaidia watu katika mambo wanayopaswa kumfanyia Mungu. Anapaswa kumtolea Mungu sadaka na sadaka za dhambi. Kuhani mkuu anao udhaifu wake binafsi. Hivyo anapaswa kuwa mpole kwa wale wanaokosea kwa sababu ya kutokujua. Hutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zao, lakini kutokana na udhaifu wake anapaswa pia kutoa sadaka kwa ajili dhambi zake mwenyewe.

Kuwa kuhani mkuu ni heshima. Lakini hayupo anayejichagua mwenyewe kwa ajili ya kazi hii. Mtu huyo anapaswa kuwa amechaguliwa na Mungu kama alivyokuwa Haruni. Ndivyo ilivyo hata kwa Kristo. Hakujichagua mwenyewe kuwa na heshima na kuwa kuhani mkuu. Lakini Mungu alimchagua. Mungu akamwambia:

“Wewe ni mwanangu.
    Leo nimekuwa baba yako.”(A)

Na katika sehemu nyingine ya Maandiko Mungu anasema:

“Wewe ni kuhani mkuu milele;
    kama Melkizedeki alivyokuwa kuhani.”(B)

Yesu alipoishi duniani alimwomba Mungu, akiusihi msaada kutoka kwa yule anayeweza kumwokoa kutoka mauti. Alimwomba Mungu kwa sauti kuu na kwa machozi. Na Mungu alizisikia sala zake kwa sababu ya heshima yake kuu kwa Mungu. Yesu alikuwa mwana wa Mungu, lakini aliteseka, na kwa njia ya mateso yake alijifunza kutii chochote alichosema Mungu. Hili lilimfanya yeye awe kuhani mkuu mkamilifu, anayetoa njia kwa ajili ya kila mmoja anayemtii ili kuokolewa milele. 10 Mungu alimfanya yeye kuhani mkuu, kama alivyokuwa Melkizedeki.

Tahadhari Kuhusu Kuanguka

11 Tunayo mambo mengi ya kuwaeleza kuhusu hili. Lakini ni vigumu kufafanua kwa sababu mmeoteza shauku ya kusikiliza. 12 Mmekuwa na muda wa kutosha ambapo sasa mngepaswa kuwa walimu. Lakini mnahitaji mtu awafundishe tena mafundisho ya Mungu ya mwanzo. Bado mnahitaji mafundisho ambayo yako kama maziwa. Hamjafikia kiwango cha chakula kigumu. 13 Yeyote anayeishi kwa kutegemea maziwa tu bado ni mtoto mchanga, hayupo tayari kuelewa zaidi kuhusu kuishi kwa haki. 14 Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu ambao wamekua. Kutokana na uzoefu wao wamejifunza kuona tofauti baina ya jema na ovu.