Kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo. Mimi nimetumwa kwa wale ambao Mungu amewateua ili niwaon goze katika imani na katika maarifa ya kweli yanayopatana na kum cha Mungu; na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo. Naye kwa wakati aliopanga alidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo nilikabidhiwa kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.

Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu

Kazi Ya Tito Kule Krete

Nilikuacha huko Krete kusudi urekebishe mambo yote yal iokuwa hayakunyooka na uchague wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. Mzee wa kanisa asiwe na lawama yo yote; awe mume wa mke mmoja; awe ni mtu ambaye watoto wake ni waamini na wala sio jeuri au wasiotii. Kwa kuwa askofu amekabidhiwa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na lawama. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyokuwa ya halali. Bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye kujitawala, mnyofu, mtakatifu na mwe nye kudhibiti na si yake. Ni lazima alishike kwa uthabiti neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine na kudhihirisha makosa ya wale wanaolipinga.

Walimu Wa Uongo

10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.

16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.