Mahubiri ya Injili huko Ikonio

14 Basi huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi. Wakahubiri kwa uwezo mkuu na umati mkubwa wa watu wakaamini, Wayahudi pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini wale Wayahudi ambao hawakupokea neno la Mungu, waliwa chochea watu wa mataifa dhidi ya wale walioamini. Paulo na Bar naba wakakaa huko kwa muda mrefu wakifundisha kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha kuwa mahubiri yao yalikuwa ni neno la neema yake; akawapa uwezo wa kutenda ishara na maajabu. Hata hivyo watu wa mji ule waligawanyika. Wengine wakaungana na wale Wayahudi na wengine wakawa upande wa mitume. Watu wa mataifa na Wayahudi walijiunga na baadhi ya viongozi wakafanya mpango wa kuwasumbua mitume na kisha kuwapiga mawe. Lakini wao walipopata habari hizi walitoroka wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya wilaya ya Likaonia, na sehemu zilizopakana nayo. Huko waliende lea kuhubiri Habari Njema.

Kiwete Aponywa Huko Listra

Katika mji wa Listra, alikuwepo kiwete amekaa, ambaye ali kuwa amelemaa miguu yote miwili tangu alipozaliwa, na hakuwahi kutembea kamwe. Alimsikiliza Paulo alipokuwa akihubiri, na Paulo alipomtazama aliona kuwa anayo imani ya kuponywa. 10 Kwa hiyo Paulo akasema kwa sauti, “Simama kwa miguu yako!” Mara yule mtu akaruka juu akaanza kutembea! 11 Wale watu walipoona maajabu aliyofanya Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao, wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!” 12 Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye alikuwa msemaji mkuu. 13 Kuhani mkuu wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua aki taka kuwatolea sadaka penye lango la mji pamoja na ule umati wa watu. 14 Lakini Paulo na Barnaba waliposikia na kuona mambo haya waliyotaka kufanya, walirarua nguo zao, wakawakimbilia wale watu, wakisema, 15 ‘ ‘Kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni binadamu tu, kama ninyi! Tumekuja kuwatangazia Habari Njema; mziache hizi ibada zisizo na maana na mumgeukie Mungu aliye hai ambaye aliumba mbingu na nchi na bahari, na vyote vilivyoko. 16 Wakati wa vizazi vilivyopita aliwaachia watu waishi walivyotaka. 17 Hata hivyo hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake. Kwa maana aliwatendea mema akawaletea mvua kutoka mbinguni na mazao kwa majira yake, akawatosheleza kwa vyakula na raha.” 18 Hata pamoja na maneno yote haya haikuwa rahisi kuwazuia wale watu waache kuwatolea sadaka zao.

19 Wakaja watu kutoka Antiokia na Ikonio wakawashawishi wale watu, wakampiga Paulo kwa mawe, wakamkokota hadi nje ya mji, wakidhani amekufa. 20 Lakini waamini walipokusanyika kumzunguka, aliamka, akarudi nao mjini. Kesho yake akaondoka na Barnaba wakaenda mpaka Derbe.

Paulo Na Barnaba Warudi Antiokia

21 Walipokwisha hubiri Habari Njema katika mji ule na watu wengi wakaamini wakawa wanafunzi, walirudi Listra na Ikonio na Antiokia. 22 Huko waliwatia nguvu wanafunzi na kuwashauri waendelee kukua katika imani. Wakawaonya wakisema, “Tunalazimika kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika mateso mengi.” 23 Na baada ya kuwachagulia wazee viongozi katika kila kanisa, wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini kwa maombi na kufunga. 24 Basi wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. 25 Na baada ya kufundisha neno la Mungu huko Perga, walikwenda upande wa kusini hadi Atalia. 26 Kutoka huko wakasafiri kwa mashua mpaka Anti okia, ambako walikuwa wameombewa neema ya Mungu kwa kazi ambayo walikuwa wameikamilisha. 27 Walipowasili Antiokia waliwakusanya waamini pamoja wakawaeleza yale yote ambayo Mungu alikuwa amewa tendea, na jinsi Mungu alivyotoa nafasi ya imani kwa watu wasio Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.