Paulo Anajitetea Mbele Ya Festo

25 Siku tatu baada ya Festo kuwasili Kaisaria kuanza kazi, alisafiri kwenda Yerusalemu. Makuhani wakuu na viongozi wa Way ahudi wakamletea mashtaka yao juu ya Paulo, na wakamwomba Festo awafanyie upendeleo, amrudishe Paulo Yerusalemu; wakiwa na mpango wa kumwua Paulo njiani. Festo akawajibu, “Paulo yuko kizuizini huko Kaisaria, na mimi natarajia kwenda huko hivi kari buni. Kwa hiyo tumeni viongozi wenu tuongozane pamoja na kama huyu mtu amefanya kosa lo lote, wao walete mashtaka yao.” Festo alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi kisha akaondoka kwenda Kaisaria. Kesho yake akakaa katika baraza la mahakama, akaamuru Paulo aletwe. Paulo alipoletwa, wale Wayahudi wal iotoka Yerusalemu walisimama wakaanza kutoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha. Lakini Paulo alijitetea, akasema, “Sikufanya jambo lo lote kinyume cha sheria za Wayahudi au Hekalu au kinyume cha Kaisari. ” Festo akitaka kuwapendeza Wayahudi, alimwuliza Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu ukahojiwe huko kuhusu mashtaka haya mbele yangu?” 10 Paulo akasema, “Mimi nasimama mbele ya baraza la mahakama ya Kaisari. Baraza hili ndilo lina wajibu wa kusikiliza kesi hii. Kama unav yojua sijawatendea Wayahudi uovu wo wote. 11 Kama mimi ni mhal ifu na nimetenda kosa linalostahili hukumu ya kifo, sijitetei ili nisiuawe; lakini kama mashtaka yao juu yangu hayana msingi, hakuna mtu atakayeweza kunitia mikononi mwao waniue. Ninakata rufaa, kesi yangu isikilizwe na Kaisari.” 12 Festo akajadiliana na baraza kisha akasema, “Umeomba rufaa usikilizwe na Kaisari; basi utakwenda kwa Kaisari.”

Paulo Afikishwa Mbele Ya Mfalme Agripa

13 Baada ya siku chache mfalme Agripa na Benike wakafika Kaisaria kumkaribisha Festo. 14 Kwa kuwa walikuwa wanakaa Kais aria kwa muda mrefu, Festo alipata nafasi ya kujadiliana na mfalme kesi ya Paulo; akamwambia, “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Feliksi alimwacha gerezani kama mfungwa. 15 Nilipokwenda Yerus alemu, makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka yao juu yake wakitaka ahukumiwe. 16 Lakini mimi niliwaambia kwamba sheria za Kirumi haziruhusu kumhukumu mtu aliyeshitakiwa kabla hajapata nafasi ya kukutana uso kwa uso na washitaki wake naye apewe nafasi ya kujitetea. 17 Walipofika hapa pamoja nami, siku kawia, bali nilikaa pamoja na baraza la mahakama nikaamuru mshta kiwa aletwe. 18 Lakini washtaki wake waliposimama, hawakutaja aina yo yote ya uhalifu kama nilivyotarajia, 19 bali walikuwa na mashtaka kuhusu mabishano fulani juu ya dini yao na juu ya mtu aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo alidai kwamba anaishi. 20 Sikujua jinsi ya kuchunguza mambo haya kwa hiyo nikamwuliza Paulo kama angelipenda kwenda Yerusalemu mashtaka haya yakasiki lizwe huko. 21 Lakini Paulo alipokata rufaa, akaomba akae kizuizini mpaka Kaisari atakapotoa uamuzi wake, niliamuru awekwe rumande mpaka nitakapompeleka kwa Kaisari.” 22 Agripa akasema, “Ningependa nimsikilize mtu huyu mwenyewe.”

Paulo Ajitetea Mbele Ya Agripa

23 Kesho yake Agripa na Bernike walifika kwa fahari kubwa wakaingia katika ukumbi wa mkutano pamoja na mahakimu wa kijeshi na watu mashuhuri wa mji. Ndipo kwa amri ya Festo Paulo akaletwa.

24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, na ninyi nyote mlio hapa pamoja nasi leo, mnamwona hapa huyu mtu ambaye Wayahudi wote wa Yerusalemu na wa hapa Kaisaria wamenisihi, wakipiga makelele kwamba hastahili tena kuishi. 25 Lakini mimi sikuona kosa lo lote alilotenda linalostahili hukumu ya kifo; na kwa kuwa yeye mwenyewe amekata rufaa kesi yake isikilizwe na Kaisari, niliamua nimpeleke kwake. 26 Lakini sina mapendekezo kamili ya kumwandi kia mtukufu Kaisari juu ya huyu mshtakiwa. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu na hasa mbele yako wewe mfalme Agripa ili baada ya kumhoji mshtakiwa nipate jambo la kuandika. 27 Kwa maana ita kuwa si jambo la busara kumpeleka mfungwa kwa Kaisari bila kuon yesha wazi wazi mashtaka yanayomkabili.”

Paulo Aomba Kumwona Kaisari

25 Festo akawa gavana na siku tatu baadaye akasafiri kwenda Yerusalemu kutoka Kaisaria. Viongozi wa makuhani na viongozi maarufu wa Kiyahudi wakatoa mashitaka dhidi ya Paulo mbele ya Festo. Walimwomba Festo awasaidie. Walitaka amrudishe Paulo Yerusalemu kwa sababu walipanga kumwua akiwa njiani. Lakini Festo alijibu, “Hapana, Paulo ataendelea kuwekwa Kaisaria. Nitaenda huko mimi mwenyewe hivi karibuni, na viongozi wenu wanaweza kufuatana nami. Kama mtu huyu hakika amefanya chochote kibaya, wanaweza kumshitaki huko.”

Festo alikaa Yerusalemu kwa siku nane au kumi zaidi kisha alirudi Kaisaria. Siku iliyofuata Festo akawaambia askari wamlete Paulo mbele yake. Festo alikuwa amekaa kwenye kiti cha hukumu. Paulo aliingia kwenye chumba na Wayahudi waliokuja kutoka Yerusalemu walisimama kumzunguka. Walileta mashitaka mengi mazito dhidi yake, lakini hawakuweza kuthibitisha chochote. Paulo alijitetea mwenyewe, akasema, “Sijatenda kitu chochote kibaya kinyume na sheria ya Kiyahudi, kinyume na Hekalu au kinyume na Kaisari.”

Lakini Festo alitaka kuwaridhisha Wayahudi. Hivyo alimwuliza Paulo, “Unataka kwenda Yerusalemu ili nikakuhukumu huko kutokana na mashitaka haya?”

10 Paulo akasema, “Kwa sasa nimesimama kwenye kiti cha hukumu cha Kaisari. Hapa ndipo ninatakiwa kuhukumiwa. Sijatenda lolote baya kwa Wayahudi na unafahamu hilo. 11 Ikiwa nilitenda chochote kibaya na sheria inasema ni lazima nife, basi ninakubali kuwa ninapaswa kufa. Siombi kuokolewa kutokana na kifo. Lakini kama mashitaka haya siyo ya kweli, basi hakuna anayeweza kunikabidhi kwa watu hawa. Hapana, Nataka Kaisari aisikilize kesi yangu!”

12 Festo alijadiliana na washauri wake kuhusu hili. Kisha akasema, “Umeomba kumwona Kaisari, basi utakwenda kwa Kaisari!”

Festo Amwuliza Mfalme Agripa Kuhusu Paulo

13 Siku chache baadaye Mfalme Agripa pamoja na dada yake aliyeitwa Bernike[a] walikuja Kaisaria kumtembelea Festo. 14 Walikaa huko kwa siku nyingi, na Festo akamwambia mfalme kuhusu kesi ya Paulo. Festo alisema, “Kuna mtu ambaye Feliki alimwacha gerezani. 15 Nilipokwenda Yerusalemu, viongozi wa makuhani na viongozi wa wazee wa Kiyahudi walitengeneza mashitaka dhidi yake. Walinitaka nimhukumu kifo. 16 Lakini niliwaambia, ‘Mtu anaposhitakiwa kuwa ametenda jambo baya, Warumi hawampeleki kwa watu wengine ili ahukumiwe. Kwanza, ni lazima aonane na watu wanaomshtaki. Na kisha ni lazima aruhusiwe kujitetea yeye mwenyewe dhidi ya mashitaka yao.’

17 Hivyo Wayahudi walipokuja hapa kwa ajili ya kesi, sikupoteza muda. Siku iliyofuata nilikaa kwenye kiti cha hukumu na kuamuru Paulo aletwe ndani. 18 Wayahudi walisimama na kumshitaki. Lakini hawakumshitaki kwa makosa niliyodhani wangemshitaki. 19 Mashitaka yao yote yalihusu dini yao wenyewe na kuhusu mtu anayeitwa Yesu. Yesu alikufa lakini Paulo anasema bado yuko hai. 20 Baada ya kuona kuwa sijui jinsi ya kuyachunguza mambo haya. Hivyo nilimwuliza Paulo, ‘Unataka kwenda Yerusalemu ili ukahukumiwe huko?’ 21 Lakini Paulo aliomba abaki mahabusu hapa Kaisaria. Anataka uamuzi kutoka kwa mfalme mkuu. Hivyo niliamua aendelee kushikiliwa hapa mpaka nitakapompeleka kwa Kaisari huko Rumi.”

22 Agripa akamwambia Festo, “Ningependa kumsikiliza mtu huyu pia.”

Festo akasema, “Utaweza kumsikiliza kesho.”

23 Siku iliyofuata Agripa na Bernike walikuja kwenye mkutano kwa fahari kubwa, wakijifanya watu wa muhimu sana. Waliingia kwenye chumba pamoja na viongozi wa kijeshi na watu maarufu wa mji. Festo akawaamuru askari wamwingize Paulo ndani.

24 Festo akasema, “Mfalme Agripa nanyi nyote mliokusanyika hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu. Wayahudi wote, hapa na Yerusalemu wamelalamika kwangu juu yake. Wanapolalamika, wanapaza sauti zao wakisema kwamba anapaswa kuuawa. 25 Nilipochunguza, sikuona ikiwa alitenda kosa lolote linalostahili hukumu ya kifo. Lakini ameomba kuhukumiwa na Kaisari, hivyo niliamua apelekwe Rumi. 26 Hata hivyo, sifahamu kwa hakika ni nini cha kumwandikia bwana wangu Kaisari kama sababu ya kumpeleka mtu huyu kwake. Hivo nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa wewe, Mfalme Agripa. Ninatumaini kwamba utamwuliza maswali na kunipa kitu cha kumwandikia Kaisari. 27 Nafikiri ni upumbavu kupeleka mfungwa kwa Kaisari bila kuainisha mashitaka dhidi yake.”

Footnotes

  1. 25:13 Bernike Dada yake Mfalme Agripa, binti mkubwa wa Herode Agripa wa Kwanza.