Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu; watu waka pata habari kuwa amerudi nyumbani. Wakakusanyika kwa wingi isibaki nafasi hata mlangoni! Naye akawahubiria. Wakaja watu wanamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. Waliposhindwa kumfikia Yesu kwa ajili ya msongamano wa watu, wakatoboa tundu darini, wakamshusha ndani yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.

Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Mwa nangu, dhambi zako zimesamehewa.” Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwepo wakawaza mioyoni mwao, “Mbona mtu huyu anasema maneno haya? Anakufuru! Hajui kuwa ni Mungu peke yake awezaye kusamehe dhambi?”

Yesu akatambua mawazo yao, kwa hiyo akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo? Ni jambo gani lililo rahisi zaidi, kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’? Au, ‘Inuka, chukua kitanda chako uende’? 10 Lakini ili kuwahakikishia kwamba mimi Mwana wa Adamu ninao uwezo hapa duniani wa kusamehe dhambi,” - akamwambia yule aliyepooza 11 “Nakuambia, inuka, chukua kitanda chako uende nyumbani.”

12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akachukua kitanda chake akatembea mbele yao wote! Tukio hili likawashangaza watu wote, wakamsifu Mungu, wakasema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”

Yesu Amwita Mathayo

13 Yesu akaenda tena kando kando ya Ziwa la Galilaya. Umati wa watu ukamfuata naye akaanza kuwafundisha. 14 Alipokuwa aki tembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi katika kibanda cha kukusanyia kodi, akamwambia, “Nifuate”. Lawi akatoka, akamfuata Yesu. 15 Yesu alipokuwa akila chakula nyumbani kwa Lawi, watoza ushuru wengi pamoja na wenye dhambi walikuwa wameketi mezani pamoja naye na wanafunzi wake; kwa maana watu wengi wa aina hii walikuwa wamemfuata. 16 Baadhi ya walimu wa sheria ambao wali kuwa Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake, “Yesu anawezaje kula na watoza ushuru na wenye dhambi?” 17 Yesu aliposikia haya aka waambia, “Wenye afya nzuri hawahitaji daktari, bali wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kuwaalika wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Afundisha Kuhusu Kufunga

18 Wakati mmoja wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wamefunga. Baadhi ya watu wakaja kwa Yesu wakamwuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na wako hawafungi?”

19 Yesu akawajibu, “Inawezekanaje wageni wa bwana harusi wafunge wakati bwana harusi yungali nao? Maadamu bwana harusi yupo, haiwezekani wafunge. 20 Lakini wakati utafika ambapo bwana harusi atachukuliwa. Siku hiyo ndipo watakapofunga.

21 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, ile nguo iliyochakaa itachanika zaidi pale penye kiraka kipya na kuharibika zaidi. 22 Wala hakuna mtu anayeweka divai mpya katika viriba vya zamani. Akifa nya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, kwa hiyo ata poteza divai na viriba pia. Divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”

Yesu Afundisha Kuhusu Sabato

23 Siku moja ya sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake, wal ikuwa wakipita katikati ya mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano. 24 Mafarisayo wakamwambia, “Mbona wanafanya jambo ambalo si halali kufanywa siku ya sabato?”

25 Yesu akawaambia, “Hamjasoma alivyofanya Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 26 Aliingia katika nyumba ya Mungu wakati Abiatha akiwa kuhani mkuu, akala mkate wa sadaka walioruhusiwa kuula ni makuhani peke yao - na akawagawia wafuasi wake.” 27 Kisha akawaambia, “Sabato iliwekwa kwa faida ya mwanadamu, lakini mwanadamu hakuwekwa kwa ajili ya sabato. 28 Na mimi, Mwana wa Adamu, ni Bwana hata wa sabato.”