Add parallel Print Page Options

14 Wakati mtakapoliona chukizo la uharibifu[a] likisimama mahali pasipotakiwa lisimame.” (Msomaji aelewe hii ina maana gani?[b]) “Kisha wale waliopo katika Uyahudi wakimbilie milimani. 15 Ikiwa mtu yupo katika paa la nyumba yake, asishuke chini na kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu chochote. 16 Ikiwa mtu yupo shambani asirudi kuchukua vazi lake.

17 Wakati huo itakuwa hatari kwa wanawake walio waja wazito na wale wenye watoto wachanga. 18 Ombeni kwamba haya yasitokee wakati wa majira ya baridi. 19 Kwa kuwa taabu itakayotokea katika siku hizo itakuwa ile ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo pale Mungu alipoumba dunia hadi sasa. Na hakitatokea tena kitu kama hicho.

Read full chapter

Footnotes

  1. 13:14 chukizo la uharibifu Ni maneno yanayoashiria kitu ambacho Mungu hapendezwi nacho. Tazama Dan 9:27; 11:31 na 12:11.
  2. 13:14 Msomaji aelewe hii ina maana gani Mwandishi anamtaka msomaji azingatie kwamba anazungumzia Jeshi la Rumi ambalo litaharibu Yerusalemu, ingawa hataki kulielezea hili kwa wazi. Tazama Lk 21:20-24.