Add parallel Print Page Options

Yesu Asafisha Eneo la Hekalu

(Mt 21:12-17; Lk 19:45-48; Yh 2:13-22)

15 Walipofika Yerusalemu waliingia katika viwanja vya Hekalu. Yesu akaanza kuwafukuza nje wale waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza na kununua katika eneo la Hekalu. Akapindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 16 Pia hakumruhusu mtu yeyote abebe kitu chochote kukatiza eneo la Hekalu. 17 Yesu akaanza kuwafundisha na kuwaeleza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko kwamba: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ambapo watu wa mataifa yote wataleta maombi yao kwangu’?(A) Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘mahali pa wezi kujificha.’(B)

18 Na viongozi wa makuhani na walimu wa Sheria waliyasikia haya, na hivyo wakaanza kutafuta njia ya kumuua. Kwani walimwogopa, kwa sababu watu wote walikuwa wamestaajabishwa na mafundisho yake. 19 Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondoka Yerusalemu.

Read full chapter