Add parallel Print Page Options

Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi

(Mt 4:18-22; Lk 5:1-11)

16 Alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa Galilaya, Yesu alimwona Simoni[a] na Andrea ndugu yake. Hao walikuwa wavuvi na walikuwa wakizitupa nyavu zao ziwani kukamata samaki. 17 Yesu akawaambia, “njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine, nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 18 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata.

19 Kisha Yesu akaendelea mbele kidogo na akawaona ndugu wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na kaka yake Yohana. Yesu aliwaona wakiwa kwenye mashua wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. 20 Naye akawaita mara moja. Hivyo wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua na watu waliowaajiri na kumfuata Yesu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:16 Simoni Jina lingine la Petro lilikuwa Simoni. Pia katika mistari wa 29,30,36.