Add parallel Print Page Options

Swali Kuhusu Kufunga

(Mt 9:14-17; Mk 2:18-22)

33 Baadhi ya watu wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohana hufunga na kuomba mara kwa mara, vivyo hivyo wafuasi wa Mafarisayo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa kila wakati.”

34 Yesu akawaambia, “Kwenye harusi huwezi kuwaambia marafiki wa bwana harusi wafunge wakati bwana harusi bado yuko pamoja nao. 35 Lakini muda ukifika na bwana harusi akaondolewa kwao. Watakuwa na huzuni, na watafunga.”

36 Yesu akawaambia mfano huu: “Hakuna anayekata kiraka kwenye vazi jipya na kukishona kwenye vazi la zamani. Ataharibu vazi jipya, na kiraka kutoka vazi jipya hakitakuwa sawa na vazi la zamani. 37 Pia hakuna mtu anayeweka divai mpya[a] katika viriba vya zamani. Divai mpya itavipasua, divai itamwagika, na viriba vitaharibika. 38 Daima mnaweka divai mpya kwenye viriba vipya. 39 Hakuna mtu ambaye baada ya kunywa divai ya zamani hutaka divai mpya. Kwa sababu husema, ‘Divai ya zamani ni nzuri.’”

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:37 divai mpya Maji ya zabibu ambayo ndiyo yanaanza kuchachuka na hutengeneza mgandamizo ndani ya chombo kilichofungwa.