Ombi Kuhusu Maombezi

Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu. Nasi tuna tumaini kubwa kwa Bwana juu yenu, kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. Bwana aielekeze mioyo yenu kwenye upendo wa Mungu na katika ustahimilivu wa Kristo.

Onyo Kuhusu Uvivu

Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu. Hatukufanya hivi kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada wenu, bali tulitaka tuwape mfano wa kuiga. 10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”

11 Tumesikia kwamba baadhi yenu ni wavivu, hawana shughuli maalumu isipokuwa kusengenya wenzao. 12 Sasa tunawaagiza na kuwaonya watu hao katika jina la Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi ili wajipatie chakula wanachokula. 13 Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema.

14 Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. 15 Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu.

Salamu Za Mwisho

16 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.

17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote.