Kutoa Kwa Ukarimu

Tunapenda mfahamu ndugu zetu, kuhusu neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia. Pamoja na majaribu makali na taabu walizopata, furaha yao na umaskini wao mkuu zimezaa utajiri wa ukarimu. Ninashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya uwezo wao hata na zaidi ya uwezo wao. Kwa hiari yao wenyewe, walitusihi wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu. Na hawakufanya tulivyotazamia bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana kwanza na ndipo wakajitoa kwetu, kufuatana na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo tulimwagiza Tito, kwa kuwa ndiye aliyeanzisha jambo hili, akamilishe kazi hii ya neema pia kwa upande wenu. Basi, kama mlivyo mbele sana katika yote: katika imani, katika kutamka, katika juhudi na katika kutupenda, hakik isheni kuwa mnakuwa wa kwanza pia katika neema hii ya kutoa.

Siwapi amri, lakini nawaonyesha jinsi wengine walivyo tay ari kutoa ili kupima ukweli wa upendo wenu. Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ingawa alikuwa tajiri, alikubali kuwa maskini kwa ajili yenu, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri. 10 Ushauri wangu kuhusu jambo hili ni huu. Ni vyema mkamilishe sasa jambo ambalo mlinia na mkaanza kulifanya tangu mwaka jana 11 ili wepesi wenu katika kunia ulin gane na kumaliza kwenu kutoa kwa kadiri ya mlicho nacho. 12 Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kufuatana na kile mtu alicho nacho, si kufuatana na kile ambacho mtu hana. 13 Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka bali pawe na uwiano. 14 Kwa wakati huu wingi wa vitu mlivyonavyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao wakiwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu. 15 Ndipo patakuwa na usawa, kama maandiko yanavyosema, “Aliyekusanya kwa wingi, hakubakiza kitu, na aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”

Tito Anatumwa Korintho

16 Tunamshukuru Mungu ambaye amempa Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali. 17 Si kwamba amekubali ombi letu tu, bali anakuja kwenu akiwa na ari na kwa hiari yake mwenyewe. 18 Pamoja naye tunamtuma ndugu ambaye anasifiwa na makanisa yote kwa huduma yake ya kuhubiri Injili. 19 Zaidi ya hayo, amechagu liwa na makanisa asafiri nasi kupeleka matoleo haya. Hii ni huduma ambayo tunafanya kwa utukufu wa Bwana na pia kuonyesha nia yetu ya kuwasaidia wengine. 20 Tumenuia kwamba mtu ye yote asiwe na sababu ya kutulaumu kuhusu jinsi tunavyosima mia matoleo haya ya ukarimu. 21 Tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunafanya haki machoni pa Bwana na machoni penu, na wala si kama sisi tuonavyo vyema. 22 Pamoja na hawa, tunamtuma ndugu yetu ambaye tumempima mara nyingi tukamwona kuwa wa kweli na mwenye juhudi, hasa zaidi sana kwa kuwa ana imani kubwa kwenu. 23 Kumhusu Tito, yeye ni mwenzangu na mfanyakazi pamoja nami kwa ajili yenu. Kuhusu hawa ndugu wengine, wao ni wawakilishi wa makanisa, nao wanamletea Kristo utukufu. 24 Kwa hiyo, waonyesheni hawa ndugu upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, ili makanisa yote yapate kuona.

Msaada kwa Watu wa Mungu Katika Uyahudi

Na sasa, kaka na Dada zetu, tunataka kuwaambia kile ambacho neema ya Mungu imefanya katika makanisa ya makedonia. Waamini hawa wamepitia katika masumbufu makubwa, na ni maskini sana. Lakini furaha yao kubwa iliwafanya kuwa wakarimu zaidi katika kutoa kwao. Ninaweza kuwaambia kwamba walitoa kulingana na uwezo wao na hata zaidi ya uwezo wao. Hakuna mtu yeyote aliyewaambia kufanya hivyo. Hilo lilikuwa wazo lao. Walituuliza tena na tena na walitusihi tuwaruhusu kushiriki katika huduma hii kwa ajili ya watu wa Mungu. Na walitoa kwa namna ambayo sisi wenyewe hatukutegemea: kwanza walijitoa wenyewe kwa Mungu na kwetu kabla ya kutoa fedha zao. Hili ndilo Mungu anataka. Kwa hiyo tulimwomba Tito awasaidie ninyi kuikamilisha kazi hii maalum ya kutoa. Tito ndiye aliyeianzisha kazi hii kwanza miongoni mwenu. Ninyi ni matajiri kwa kila kitu; katika imani, katika uwezo wa kuzungumza, katika maarifa, katika utayari wa kusaidia kwa njia yo yote, na katika upendo mliojifunza kutoka kwetu. Hivyo sasa tunawataka muwe matajiri katika kazi hii ya kutoa pia.

Siwashurutishi ninyi kutoa, ila nataka niujaribu upendo wenu kuona ni wa kiasi gani kuwalinganisha na wengine ambao wamekuwa tayari na wana hiari ya kusaidia. Mnaifahamu neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mnafahamu kuwa aliacha utajiri wake mbinguni na kufanyika maskini kwa ajili yenu. Aliacha kila kitu ili ninyi mbarikiwe kwa wingi zaidi.

10 Hili ndilo ninafikiri mnapaswa kufanya: mwaka jana mlikuwa wa kwanza kutaka kutoa, na mkawa wa kwanza kutoa. 11 Hivyo sasa ikamilisheni kazi mliyoianzisha. Kisha kutenda kwenu kutakuwa sawa na “kutaka” kwenu “kutenda”. Toeni kutokana na kile mlicho nacho. 12 Ikiwa mnataka kutoa, sadaka yenu itapokelewa. Sadaka yenu itahukumiwa kutokana na kile mlicho nacho, si kwa kile msichonacho. 13 Hatupendi muwe na mizigo wakati wengine wanastarehe. Tunataka kila kitu kiwe katika hali ya usawa. 14 Wakati huu mnavyo vingi na kuzidi na mnaweza kuwapa kila wanachohitaji. Kisha baadaye, watakapokuwa navyo vingi, wataweza kuwapa mnavyohitaji. Kisha kila mmoja atakuwa na mgao ulio sawa. 15 Kama Maandiko yanavyosema,

“Wale waliokusanya vingi hawakuwa na vingi zaidi,
    na wale waliokusanya kidogo hawakuwa na vichache zaidi.”(A)

Tito na Wale Watakaosafiri Pamoja Naye

16 Namshukuru Mungu kwa sababu alimpa Tito upendo ule ule nilionao mimi kwenu. 17 Tito alikubali kufanya vile tulivyomwomba. Yeye mwenyewe alitamani sana kuja kwenu. 18 Tunamtuma Tito pamoja ndugu anayekubalika katika makanisa yote. Anasifiwa kwa sababu ya huduma yake ya Habari Njema. 19 Pia, alichaguliwa na makanisa kuambatana nasi tunapoleta sadaka hii. Tunafanya huduma hii kumpa Bwana heshima[a] na kuonesha kuwa tunapenda kusaidia.

20 Tunajitahidi kuwa waangalifu ili asiwepo mtu wa kutukosoa kwa namna ambavyo tunashugulika na sadaka hii kubwa. 21 Tunajaribu kutenda lililo jema. Tunataka kufanya kile ambacho Bwana anakubali kuwa sahihi na kile ambacho watu wanafikiri kuwa ni sahihi.

22 Pia, tunawatuma pamoja nao kaka yetu ambaye yuko tayari siku zote kutoa msaada. Amethibitisha hili kwetu mara nyingi na kwa njia nyingi. Na anataka kusaidia zaidi sasa kwa sababu ana imani zaidi nanyi.

23 Na sasa kuhusu Tito, yeye ni mshirika mwenzangu. Anafanya kazi pamoja nami kuwasaidia ninyi. Na kuhusu hawa kaka wawili wengine: wao wametumwa kutoka katika makanisa mengine, na wanaleta heshima kwa Kristo. 24 Hivyo waonesheni watu hawa kuwa mna upendo. Waonesheni kwa nini tunajisifia ninyi. Ndipo makanisa yote yatakapo tambua hili.

Footnotes

  1. 8:19 heshima Au “utukufu”. Tazama Utukufu katika Orodha ya Maneno.