Maagizo Kuhusu Ibada

Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia. Jambo hili ni jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu ambaye anapenda watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli. Maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wote. Yeye ni uthibitisho wa mambo haya, uliotolewa kwa wakati wake. Na hii ndio sababu nilichaguliwa niwe mhubiri na mtume, nasema kweli sisemi uwongo; nilichaguliwa niwe mwalimu wa watu wa mataifa katika imani na kweli.

Kwa hiyo, nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono iliyotakaswa pasipo hasira wala mabishano. Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu na mavazi ya gharama kubwa, 10 bali kwa matendo mema kama iwapa savyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu. 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu na unyenyekevu.

12 Simruhusu mwanamke ye yote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya. 13 Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza kisha Hawa; 14 na Adamu hakudanganywa bali mwanamke alidanganywa akawa mkosaji. 15 Lakini mwanamke ataoko lewa kwa kuzaa, kama ataendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kujiheshimu.

Mungu Anataka Tumwombee Kila Mtu

Kwanza kabisa, ninakuagiza uwaombee watu wote. Uwaombee kwa Mungu ili awabariki na kuwapa mahitaji yao. Kisha umshukuru Yeye. Unapaswa kuwaombea watawala na wote wenye mamlaka. Uwaombee viongozi hawa ili tuweze kuishi maisha yenye utulivu na amani, maisha yaliyojaa utukufu kwa Mungu na yanayostahili heshima. Hili ni jambo jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu.

Mungu anataka kila mtu aokolewe na aielewe kweli kikamilifu. Kuna Mungu mmoja tu, na kuna mwanadamu mmoja tu anayeweza kuwaleta pamoja wanadamu wote na Mungu wao. Huyo mtu ni Kristo Yesu kama mwanadamu. Alijitoa mwenyewe kulipa deni ili kila mtu awe huru. Huu ni ujumbe ambao Mungu alitupa wakati unofaa. Nami nilichaguliwa kama mtume kuwaambia watu ujumbe huo. Ninasema kweli. Sidanganyi. Nilichaguliwa kuwafundisha wasio Wayahudi na nimefanya kazi hii kwa imani na ukweli.

Maagizo Maalumu kwa Wanawake na Wanaume

Nataka wanaume walio kila mahali waombe. Ni lazima wawe watu wanaoishi kwa kumpendeza Mungu na wanaonyoosha mikono yao wanapoomba na wawe watu wasio na hasira na wanaopenda mabishano.

Na ninawataka wanawake wajipambe kwa namna inayofaa. Mavazi yao yawe yanayofaa na yanayostahili. Hawapaswi kuvutia watu kwa kutengeneza nywele zao kwa mitindo ya ajabu ama kwa kuvaa dhahabu, vito au lulu au nguo za gharama. 10 Lakini wajipambe na kuvutia kwa matendo mema wanayofanya. Hayo ndiyo yanayofaa zaidi kwa wanawake wanaosema kuwa wamejitoa kwa ajili ya Mungu.

11 Mwanamke anapaswa kujifunza akisikiliza kwa utulivu huku akiwa radhi kutii kwa moyo wake wote. 12 Simruhusu mwanamke kumfundisha mwanaume au kumwelekeza jambo la kufanya. Bali lazima asikilize kwa utulivu, 13 kwa sababu Adamu aliumbwa kwanza na Hawa akaumbwa baadaye. 14 Na Adamu hakudanganywa.[a] Bali mwanamke ndiye aliyedanganywa naye akatenda dhambi. 15 Lakini wanawake wataokolewa kwa jukumu lao la kuzaa watoto.[b] Wakiendelea kuishi katika imani, upendo, utakatifu na tabia njema.

Footnotes

  1. 2:14 Adamu hakudanganywa “Adamu siye aliyedanganywa” Shetani alimdanganya Hawa, naye Hawa alisababisha Adamu kutenda dhambi. Tazama Mwa 3:1-13.
  2. 2:15 kuzaa watoto Kwa maana ya kawaida, “Ataokolewa katika kazi yake ya kuzaa watoto.” Kuzaa watoto, inaweza kutumika hapa kama kielelezo cha maana ya “kuzaa sifa njema”, zinazofafanuliwa katika mstari unaofuata.